Hifadhi Picha za Zamani za Familia Yako Kabla Hazijapotea
Kila mmoja ana picha za zamani za familia zilizotunzwa ndani ya makabati, albamu na kwenye chumba kidogo juu ya dari. FamilySearch hufanya iwe rahisi kuhifadhi, kupangilia na kushiriki picha, hadithi na nyaraka za mababu zako ili ziweze kufurahiwa kwa vizazi vingi.
Jinsi Inavyofanya Kazi
Badilisha picha za zamani za familia kuwa kumbukumbu za familia zilizohifadhiwa katika hatua chache tu.
Pakia picha ya zamani ya familia
Piga picha au skani picha yoyote ya zamani ya familia, hata kama imefifia, imechanika au imepachikwa kwenye albamu iliyochakaa.
Ongeza majina na maelezo
Watagi watu kwenye picha, ongeza tarehe, mahala na hadithi na unganisha picha kwa babu anayehusika.
Ishiriki na familia yako
Mara picha yako inapokuwa imepakiwa, ndugu wanaweza kuigundua, kuifurahia na kuongeza taarifa za ziada kwenye hadithi ya pamoja ya familia.
Zaidi ya Picha Tu
FamilySearch Memories inakusaidia kuhifadhi zaidi ya picha. Unaweza pia kuongeza hadithi, kumbukumbu na sauti ambazo huileta historia ya familia yako kwenye uhai.
Picha
Pakia picha za familia yako na mababu zako, iwe zimeskaniwa, zimepigwa au tayari ziko katika mfumo wa kidijitali.
Nyaraka
Hifadhi barua, shajara, vyeti, maelezo ya upishi, nyaraka za jeshi zilizoskaniwa na kumbukumbu zingine za familia.
Hadithi
Andika katika hadithi za familia, kumbukumbu na maelezo ambayo yanatoa ufafanuzi wa mababu zako walikuwa akina nani na kile kilichokuwa muhimu kwao.
Sauti
Rekodi au pakia sauti za wazazi, bibi na babu na ndugu wakisimulia hadithi zao kwa maneno yao wenyewe.
Albamu
Tumia albamu kwa mikusanyiko ya kumbukumbu zinazohusiana.
Anza Leo
Tumia vipengele hivi vyenye nguvu ili kuhifadhi na kushiriki kumbukumbu zako za thamani.
Kwa Nini Uchague FamilySearch Memories?
app nyingi zinaweza kuhifadhi picha. FamilySearch Memories imekusudiwa kuhifadhi historia ya familia katika njia ambazo hakuna huduma nyingine inaweza.
Ni ya bila malipo na imetunzwa kwa ajili ya vizazi vijavyo
Kumbukumbu za kihistoria mara nyingi zinaweza kufunua maelezo muhimu kuhusu wapi familia yako waliishi.
Imepangiliwa kuzunguka watu na hadithi
Tofauti na app ya picha ya kundi, FamilySearch huunganisha picha, nyaraka, hadithi na sauti moja kwa moja kwa watu katika mti wa familia yako.
Imeunganishwa kwenye mti jumuishi wa familia
Ndugu wa mbali yawezekana tayari amepakia picha, hadithi au kumbukumbu kuhusu mababu zako.
Ni salama na rafiki kwa familia
FamilySearch hutumia viwango vyenye heshima vya maudhui na hutunza kumbukumbu za watu walio hai kuwa za binafsi.
Unakuwa katika udhibiti
Chagua ikiwa kumbukumbu ni ya umma, binafsi au ya kushirikiwa kwenye kundi. FamilySearch haiuzi data zako.
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara
Usiruhusu Picha za Zamani za Familia Yako Zibaki Zimefichwa!
Hadithi kuhusu picha zako ni za muhimu sana! Zihifadhi sasa ili familia yako iweze kuzifurahia kwa vizazi vingi.