Dhamira Yetu ya Upatikanaji
Tunajitolea kuhakikisha kwamba nyenzo zetu za vizazi zinapatikana kwa watu wote, ikijumuisha wale wenye ulemavu.
Upatikanaji kutokea Chini hadi Juu
FamilySearch hujumuisha upatikanaji kwenye ubunifu na maendeleo ya tovuti yetu na aplikesheni. Tunajitahidi kuendana naMiongozo ya Upatikanaji wa Maudhui ya Tovuti (WCAG)ili kuhakikisha kwamba majukwaa yetu yanafahamika, yanafanya kazi, yanaeleweka na imara. Kwa dhati tunahitaji maoni ya mtumiaji ili kutambua maeneo ya kuboresha na mara kwa mara kukuza uwezo wa vifaa vyetu vya kidijitali ili kuzitumikia familia vyema zaidi ulimwenguni kote.
Vipengele vya Upatikanaji
Ili kuunga mkono mahitaji tofauti, FamilySearch hutoa vipengele kama:
- Utangamano wa Kisoma Skrini kwa watumiaji ambao ni vipofu au wenye uoni hafifu.
- Msaada wa matumizi ya kibodi kwa watumiaji wenye madhaifu ya kimwili.
- Maelezo mafupi kwenye video kwa watumiaji wenye shida ya kusikia.
- Miundo inayoweza kupatikana kwa ajili ya kumbukumbu ya vizazi na nyenzo, ikijumuisha ongezeko la idadi ya picha zenye maneno yanayoweza kunakiliwa.
Tunaendeleaje?
Kama utapitia changamoto za upatikanaji wakati ukitumia tovuti yetu au aplikesheni au kama una mapendekezo kwa ajili ya kukuza uzoefu, tafadhali wasiliana nasi kwenyesupport@FamilySearch.org. Maoni yako hutusaidia kuifanya FamilySearch.org kuwa bora zaidi kwa wageni wote wa tovuti.
Msaada wa Mawasiliano